Back to top

WATUMISHI KUJIPIMA VVU, KAZINI

13 January 2023
Share

Serikali imesema imeanzisha huduma ya kujipima Virusi Vya Ukimwi (VVU), mahala pa kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa watumishi makazini hasa wanaume, ambapo hadi kufikia Disemba 2022, watu wapatao 96,231 wamepatiwa huduma ya JIPIME mahala pa kazi.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, wakati akiwasilisha taarifa kuhusu kuhuisha na kujumuisha maswala ya UKIMWI mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI