Back to top

MAONI CHAMA CHA WAUGUZI SIO MSIMAMO WA WIZARA

13 January 2023
Share

Wizara ya Afya imesema, maoni yaliyotolewa na Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA), kufuatia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwahusisha Bi.Rose Shirima (Muuguzi na Mkunga) na Bw.James G. Chuchu (Mteknolojia Maabara), watumishi wa Zahanati ya Ishishimulwa iliyopo wilayani Uyui, mkoani Tabora, waliokuwa wakijibizana (bila staha) kuhusu matumizi ya kipimo cha haraka cha kupima malaria (MRDT) kinachodaiwa kuisha muda wake, siyo msimamo wa Wizara ya Afya bali ni maoni yao kama chama hiari cha kitaaluma.
.    
Hata hivyo, Wizara hiyo imesema uchunguzi wa suala hilo unaendelea kwa ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI, na mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya serikali.