Back to top

HAKIJACHUKULIWA KIUNGO KABURI LILILOFUKULIWA

06 April 2023
Share

Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa, kaburi lililoripotiwa kufukuliwa hivi karibuni, wilayani Manyoni, uchunguzi umebaini kuwa, kilichochukuliwa kwenye kaburi hilo ni nguo, cheni, saa, pete na viatu vya marehemu na hakuna kiungo kilichochukuliwa kama taarifa zinavyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii.  
.
Jeshi hilo limesema, matukio ya kishirikina kwenye Wilaya hiyo, yanaongozwa na imani potofu  ambazo ni aibu na pia ni uhalifu.