
Kufuatia kuvuja kwa nyaraka za siri za kijeshi za Marekani, Idara ya upelelezi nchini humo (FBI), limetangaza kukamatwa kwa Jack Teixeira (21), ambaye ni mfanyakazi kwenye kitengo cha ujasusi cha kikosi cha usalama wa anga katika jimbo la Massachusetts, akihusishwa na uvujaji huo.
.
Teixeira amekamatwa kwenye makazi yake yaliyopo katika Mji wa North Dighton, Jimbo la Massachusetts, Alhamisi alasiri.
