Back to top

JINA PELE LAWEKWA KWENYE KAMUSI KAMA KIVUMISHI

27 April 2023
Share

Kamusi ya Brazil imeliongeza jina la utani la mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu nchini humo, 'Pele' kama neno la kivumishi cha kutumia wakati wa kufafanua mtu ambaye ni wa 'kipekee' au 'asiye wa kawaida' ambaye hawezi kulinganishwa na kitu chochote au mtu yeyote, mfano: Yeye ni pele wa mpira wa vikapu.


Bingwa huyo mara tatu wa Kombe la Dunia, ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, alifariki Disemba, 2022 akiwa na umri wa miaka 82 kutokana saratani ya utumbo.