
Mchungaji Ezekiel Odero wa Kanisa la New Life Prayer Center nchini Kenya, ameachiwa huru baada ya kushikiliwa na Polisi kwa wiki moja, akishutumiwa kuwa na uhusiano na Mchungaji Paul Nthenge Mackenzie, anayekabiliwa na mashtaka ya ugaidi kutokana na vifo vya zaidi ya watu 100 ambao inadaiwa aliwaamuru wafunge hadi kufa.
.
Odero ameachiwa leo Alhamis Mei 04, 2023, na Mahakama ya Mombasa kwa bondi ya Ksh. mil. 3 au dhamana ya Ksh. mil 1.5 pesa taslimu, ambapo alipokelewa na wafuasi wake waliokuwa wakiimba "si uchawi, ni maombi" huku akitakiwa kuripoti polisi mara moja kila wiki na amezuiwa kutoa maoni yake kuhusu mauaji ya Shakahola.