Back to top

WALIMU WAHUSISHWA NA BIASHARA NGONO

08 May 2023
Share

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera ,wameomba kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa walimu 6 wa shule ya Sekondari ya Nyankatala, wakiwatuhumu kuwashawishi wanafunzi wa kike kuingia kwenye biashara za ngono, hali ambayo wamedai inasababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kwenye shule hiyo.
.
Madiwani hao wametoa ombi hilo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ,wakati wakijadili hoja mbalimbali, ambapo wamesema wanashangazwa kuona hatua hazichukuliwi licha ya kuundwa kwa Tume ya Awali ya Uchunguzi.