
Watumishi wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) wamekumbushwa kuzingatia viwango vya juu vya uadilifu, nidhamu na kutoa huduma bila upendeleo kwa kila mmoja ili kutimiza malengo ya taasisi hiyo, kuepuka upendeleo na kutoa huduma chini ya kiwango.
Wito huo umetolewa na Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Fabian Pokela katika mafunzo ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yaliyofanyika jijini Mwanza.
“Uadilifu katika kutekeleza majukumu yetu ni chachu ya maendeleo kwa jamii yoyote ile, takriban nchi zote zilizofanikiwa, zimekuwa na viwango vya juu vya uadilifu katika kutimiza malengo yao" Amesema Bw. Pokela.
Awali akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa TTB Bw. Stanley Mnozya amesema kuwa wao kama Bodi wameandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuwakumbusha watumishi misingi ya maadili katika utumishi wa umma kwani ndio ufunguo katika kutekeleza majukumu ya kila siku.