
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa washauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii) wanne, akiwemo Mhe.William Lukuvi - Mbunge wa Jimbo la Ismani, Bw.Abdallah Bulembo - Mbunge Mstaafu, Balozi Rajab Omar Luhwavi - alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji na Bw.Haji Omar Kheir - Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
