Back to top

SHULE YA MSINGI DARAJANI YAKABILIWA NA UCHAKAVU WA MADARASA

14 June 2023
Share

Shule ya Msingi Darajani iliyopo wilayani Muheza, mkoani Tanga, inakabiriwa na changamoto ya uchakavu wa madarasa na upungufu wa matundu ya vyoo, ambayo baadhi kuta zake zimepata ufa huku mengine yakivuja, hali ambayo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw.Nyenga Abdallah Nyenga amedai kuwa imekuwa ikisababisha wanafunzi kusghindwa kusoma kwa kuhofia madaftari yao kuloana.
.
Kufuatia adha hiyo ITV imemtafuta Afisa Elimu ya Msingi mkoani humo, Bi.Pili Maximilian. ambaye amesema changamoto hiyo wanaifahamu na tayari serikali imetenga bajeti kufanya ukarabati wa shule chakavu wiloayani humo.