
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, amewataka watanzania kupuuza upotoshaji kuhusu mkataba wa bandari, ambapo amesema kuwa serikali haiwezi kufanya maamuzi yatakayowaumiza wananchi wake.
.
Chongolo ameyasema hayo leo Juni 15, 2023 kwenye ziara yake ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama hicho, mkoani Dodoma.
