
Jeshi la Polisi nchini limekamata mifugo 319 iliyokuwa imeibiwa kwenye maeneo mbalimbali hapa Nchini, katika kipindi cha mwezi Juni 2023, huku likibainisha kuwa watuhumiwa 153 wanaohusishwa na wizi huo wamekamatwa na tayari wamefikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.
.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini, ACP Simon Pasua, alipotembelea mnada wa Kikatiti uliopo wilayani Arumeru,
Mkoani Arusha, ambapo amebainisha kuwa kikosi hicho kwa kushirikiana na wananchi wameunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kutokomeza wizi wa mifugo hapa nchini.
