
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu, amewataka Wafamasia nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi yao ikiwemo kuacha kutoa dawa kwa wagonjwa wasiokuwa na cheti cha daktari, kwa dawa zenye uhitaji wa kuwa cheti hicho, ili kuepuka usugu wa dawa kwa wagonjwa hao.
.
Mhe.Ummy ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafamasia na Mkutano wa 14 wa Mwaka wa Chama cha Wanafunzi Wafamasia nchini (TAPSA), yaliyofanyika Jijini Dodoma.
