Back to top

JOTO LAZIDI INDIA, WATU 100 WAFARIKI

19 June 2023
Share

Karibu watu 100 wamefariki dunia nchini India, kutokana na joto kali lililolikumba taifa hilo.

Watu hao wamefariki dunia katika majimbo mawili yenye idadi kubwa zaidi ya watu ya Uttah Pradesh magharibi mwa nchini hiyo na Bihar, lililoko upande wa Mashariki.

Maofisa wa afya wamewataka wakazi maeneo hayo hasa wa kuanzia miaka sitini na wenye maradhi mbalimbali wakae ndani nyakati za mchana.

Serikali imesema waliofariki dunia ni wazee wa zaidi ya miaka sitini na wenye matatizo ya kiafya na huenda joto kali lilichochea vifo vyao.