Back to top

MCHIMBAJI WA MADINI AFARIKI HUKO KENYA

20 June 2023
Share

Mchimba wa madini mwenye umri wa miaka 45, James Robi Nyahure, amefariki dunia katika mgodi wa dhahabu katika Kijiji cha Kurutyange, Kuria Magharibi, kaunti ya Migori, huko Kenya.

Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Kuria Magharibi, Cleti Kimaiyo amethibitisha na kusema uchunguzi wa awali umebaini marehemu alikuwa na kifafa na wanashuku kuwa huenda alipatwa na kadhia hiyo akiwa ndani ya mgodi huo.

Kamanda Kimaiyo amesema mwili wa mchimbaji huyo, umehifadhiwa katika hospitali ndogo ya Kuria West, huku akitoa wito kwa wachimbaji kuwa waangalifu wanapokuwa katika shughuli zao ili kuepusha vifo, na pia kufanya tathmini ya usalama wa migodi hiyo kabla ya kuingia ndani.