Back to top

MAANDALIZI DAFTARI LA FIDIA KWA WANANCHI KILWA

20 June 2023
Share

Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya uwekaji wa wazi wa daftari la fidia kwa wananchi, wanaopisha upanuzi wa kiwanja cha ndege cha kilwa masoko ambacho kinataka kuanza kujengwa kwa viwango vya ujenzi wa kisasa.

Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete, ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali ka Mbunge wa Kilwa Kusini Mhe.Ally Kassinge aliyetaka kujua lini serikali itawalipa fidia wananchi 144 wa Kilwa Masoko, ambao maeneo yao yalifanyiwa tathimini kwa lengo ka kupisha upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Kilwa Masoko.

Mhe.Mwakibete katika majibu yake ya msingi amesema serikali ilishafanya uthamini wa mali za wananchi kwa kipindi cha robo ya kwanza ha mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo idadi ya wananchi iliongezeka kutoka 44 waliofanyiwa tathimini mwaka 2013 kutoka 44 hadi kufikia wananchi 438.