Back to top

WASHUSHA TRANSFOMA 2 NA KUIBA KOPA, SIMIYU

20 June 2023
Share

Watu wasiojulikana wameharibu miundombinu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), mkoani Simiyu, kwa kushusha transfoma mbili, zilizopo katika vijiji vya Kasoli na Kilalo, wilayani Bariadi kisha kuchukua nyaya za kopa, na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme na maji kwenye vijiji hivyo.
.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi wilayani humo kwa kushirikiana na TANESCO, limesema tayari linawashikilia watu wanne amabo wamekutwa na nyaya hizo.