Back to top

HAKIKISHENI MNAONGOZWA NA SHERIA ZA UCHAGUZI - NEC

21 June 2023
Share

Wasimamizi wa uchaguzi wa Kata zinazotarajiwa kufanya uchaguzi mdogo wa madiwani, mnamo Julai 13, 2023, wametakiwa kuhakikisha wanaongozwa na katiba, sheria za uchaguzi na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), katika kutekeleza majukumu yao.

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo.


Maelekezo hayo yametolewa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi hao, yaliyofanyika mjini Iringa, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi huo wa Madiwani katika kata 14 za Tanzania Bara. 
.
Aidha, Mjumbe huyo amewakumbusha wasimamiz hao kuwa, jukumu lililo mbele yao ni kubwa na linahitaji umakini na kujitoa, hivyo wazingatie umahiri, umakini na weledi katika kutekeleza jukumu hilo, ikiwemo kupata watendaji wa vituo wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo muhimu.