Back to top

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO ALIYETOWEKA, AKUTWA MBALIZI

23 June 2023
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema limempata mwanafunzi, aitwaye Ester Noah, anayesoma shule ya sekondari Panda Hill, kidato cha 5, mchepuo wa PCB, aliyedaiwa kupotea Mei 18, 2023.
.
Akitoa Taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Benjamin Kuzaga, amesema mwanafunzi huyo amekutwa katika maeneo ya Ifisi, Mji Mdogo wa Mbarizi ambapo alikuwa kwenye chumba cha kupanga cha mwanamke mmoja, ambaye ni mfanyabiashara wa genge.
.
Jeshi hilo limesema, kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo, binti huyo alipelekwa kwake na kijana aliyemfahamu kwa jina la Baba Jose ambaye amedai ni mteja wake anayemuuzia mkaa, ambapo alimweleza kuwa binti huyo ni mke wake, ametoka nae mkoani Morogoro, hivyo alimuomba ampe hifadhi wakati yeye akitafuta chumba cha kupanga.