
Watu 3890 waliogundulika kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu na Virusi Vya Ukimwi, mkoani Mtwara, wametoroka na kuacha kutumia dawa, hali ambayo wataalamu wa afya mkoani humo wamesema inaweza kuwaletea athari mbalimbali wagonjwa hao ikiwemo dawa kuwa na usugu na kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
.
Akitoa taarifa hiyo kwa uongozi wa serikali ya Mkoa wa Mtwara na viongozi wa dini Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dr.Ahmad Nyembea amesema idadi hiyo ni kubwa na inatakiwa irudi ili iendelee kupata tiba.
.
Aidha, Dr.Nyembea amewaomba viongozi wa dini kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuuelimisha umma, ikiwa ni pamoja na kuwaondoa hofu na kuwaeleza umuhimu wa kutumia dawa ili waweze kuendesha maisha yao.
