Back to top

VITUO MAALUM KWA AJILI YA WATOTO VYAONGEZWA

28 June 2023
Share

Serikali imeongeza vituo vyenye vyumba maalumu kwa ajili ya kutoa huduma kwa watoto wachanga wenye umri kati ya sifuri mpaka mitano wenye hali mahututi (Neonatal Intensive Care Unit), kutoka 18 mwaka 2017 hadi 175 mwaka 2023, ikiwa ni hatua ya serikali kupunguza vifo vya watoto wenye umri 0 hadi 1.
.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu maswali Bungeni Jijini Dodoma, ambapo pia amebainisha kuwa wameendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma juu ya namna ya kutoa huduma jumuishi kwa watoto wachanga na watoto wakubwa (Intergrated Management of Childhood Illness-IMCI) ili kuokoa vifo vya watoto hao vinavyoweza kuepukika.