Back to top

MA-DED WAPEWA SIKU MBILI KUPELEKA FEDHA WALIZOKUSANYA KWA POS, BENKI

28 June 2023
Share

Wakurugenzi wa Halmashauri nchini ambazo zimekusanya mapato kupitia mfumo mpya wa TAUSI na hawajapeleka fedha hizo benki wametakiwa kuhakikisha  zinapelekwa benki, ndani ya siku mbili, kabla ya mwaka wa fedha 2022/23 kuisha.
.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI, Mhe. Deo Ndejembi, katika Kikao na Idara ya Serikali za Mitaa, kwa ajili ya kupokea taarifa ya hali ya ukusanyaji na usimamizi wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo amebainisha kuwa hadi kufikia Juni 25, 2023, kiasi cha Shilingi bilioni 2.4 zilizokusanywa kupitia POS katika mfumo wa ukusanyaji wa mapato wa TAUSI kwenye halmashauri zilikuwa hazijapelekwa benki lakini kwenye mfumo zinaonekana zimekusanywa.
.
Aidha, Ndejembi ameziagiza Halmashauri 103 ambazo hazijafanya Usuluhishi wa Kibenki (Bank Reconciliation) ambao unatakiwa kufanyika ndani ya siku 15 baada ya mwezi kuisha kuhakikisha wanafanya ndani ya siku mbili ili kuepuka hoja za CAG.