Back to top

MSIWE NA HOFU, SERIKALI INA NIA NJEMA - MAJALIWA

29 June 2023
Share

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa, amewatoa hofu wananchi, kuhusu uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam, kwani malengo ni kuboresha uchumi wa Tanzania na kuwarejesha watumiaji walioihama bandari hiyo, ambapo pia ameeleza kuwa bandari ya Dar es Salaam ni kitovu cha uchumi, na mwekezaji anayekuja ana uzoefu mkubwa na teknolojia ya hali ya juu katika uendeshaji shughuli za bandari kwenye nchi 68.
.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo, Juni 29, 2023, wakati akizungumza na waumini waliohudhuria swala ya kitaifa ya Eid el Adh’haa iliyofanyika kwenye msikiti wa Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco, Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, ambapo alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
.
Aidha, Mhe.Majaliwa, amesema mjadala unaoendelea kuhusu uwekezaji huo, usiligawe Taifa kwa sababu Serikali ya awamu ya sita ni sikivu na inapokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau na ina nia njema kuhusu suala hilo na ndiyo maana ililiweka hadharani.