
Wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wanasayansi wa mambo ya anga, wameiomba serikali kuongeza hamasa ya kuvitangaza vivutio vya utalii, vinavyotokana na anga, kikiwemo kimondo cha Mbozi, ambacho ni cha kwanza kwa ukubwa nchini, hali ambayo wamesema itasaidia kuongeza idadi ya watalii nchini.
.
Wadau hao wameyasema hayo, walipokutana mkoani Songwe, kujadili namna ya kukuza utalii huo, ikiwa ni kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani, ambayo kitaifa yatafanyika wilayani Mbozi.
