Back to top

RC ARUSHA: WANAOHUJUMU MIRADI WAKAMATWE

30 June 2023
Share

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.John Mongela, ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama, wilayani Karatu, inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw.Dadi Kolimba, kufanya uchunguzi na kuwakamata, baadhi ya watumishi wanaodaiwa kuhujumu fedha za miradi ya maendeleo.
.
Mongela ametoa agizo hilo, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kilichokaa kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/2022, huku akisisitiza kuwa haiwezekani Rais ateseke  kutafuta hela alafu watu wafanye upuuzi. 
.
"DC anzisha oparesheni, hizo qutation zote hata...za zamani ambazo zimekuwa inflated, wakusanye tu hata kama wamemaliza kujenga darasa, tukithibitisha we wakusanye tu...kwani kule magereza tunawachaji?" John Mongela - Mkuu wa Mkoa wa Arusha