Back to top

META KUZINDUA PROGRAM INAYOFANANA NA TWITTER ITAITWA 'THREADS'

04 July 2023
Share

Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp, iko mbioni kuzindua program inayofanana na mtandao wa Twitter, huku ikitajwa kuwa ni mpango wa kuleta ushindani kwa Twitter.
.
Program hiyo itakayojulikana kwa jina la 'Threads' inatarajiwa kuzinduliwa siku ya Alhamis, na itapatikana kwenye App Store na itaunganishwa na Instagram, huku ikitajwa kuwa itatumika bila malipo na haitakuwa na vizuizi kama ambavyo vimetambulishwa na Twitter hivi karibuni.


Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita Mmiliki wa Kampuni ya META, Mark Zuckerberg na Mmiliki wa Kampuni ya Twitter Elon Musk walikubaliana kupigana kwenye ulingo wa Vegas Octagon, uliopo Las Vegas, nchini Marekani, ingawa mpaka sasa haijulikani kama kweli mabilionea hao walikuwa na nia ya kufanya pambano hilo.
.
Wakati META ikitarajia kufanya uzinduzi huo, Twitter imewatangazia watumiaji wa bidhaa yake ya TweetDeck kuwa wataanza kuilipia ndani ya siku 30.