Back to top

MKOA WA KIGOMA KUPATA AMBULANCE 17 - DKT.MOLLEL

04 July 2023
Share

Serikali imesema, Mkoa wa Kigoma utapata magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) 17, zitakazosaidia kutatua changamoto ya huduma za Rufaa pamoja na vifo vya mama na mtoto kwenye Mkoa huo, huku ikibainisha kuwa tayari imenunua jumla ya magari ya kubebea wagonjwa 727 ambayo inatarajia kuyagawa nchi nzima.
.
Kauli imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu, pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma.
.
Aidha, Dkt. Mollel ametoa pongezi kwa watoa huduma wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Maweni kwa jitihada na ubunifu wanaoendelea kuonyesha katika kuboresha huduma kwa wananchi, hali ambayo amesema imepunguza Rufaa za wagonjwa ndani ya Mkoa huo kwa zaidi ya 28% ndani ya muda mfupi, huku malengo yakiwa kupunguza zaidi ya 90%.