Back to top

NYAMA ‘KIBUDU’ YAFUKIWA MKURANGA PWANI

07 July 2023
Share

Serikali wilayani Mkuranga mkoani Pwani, imeamuru kufukiwa nyama ya ng’ombe aliyekufa ghafla, baada ya mmiliki wake kutoa tangazo la  kutaka kuiuza nyama hiyo, kwa wafugaji wa mbwa maeneo yanayozunguka Kata ya Mwandege, akidai kuwa nyama hiyo inafaa kwa mbwa.


Amri hiyo imetolewa, ili kunusuru afya za baadhi ya wananchi ambao wangejaribu kula nyama, hiyo ambayo ni mfugo uliokufa (Kibudu).


Kaimu mkuu wa wilaya ya Mkuranga  Meja Edward Gowelle ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Rufiji, amethibitisha nyama hiyo kufukiwa chini ya uangalizi wa mkaguzi wa kata  hiyo, eneo la Vicheji Katalukumbi, kata ya Mwandege Mkuranga Pwani.

Serikali imeshtuka baada ya kituo pendwa cha ITV kutaka kujua kuzagaa kwa tangazo hilo kwenye makundi tofauti ya whatapp wilayani Mkuranga,   likieleza nyama hiyo itauzwa kwa bei ya kilo shilingi elfu mbili, kwa wale wanaofuga mbwa kata ya Mwandege Mkuranga.