Back to top

KASI UTOAJI ELIMU MKATABA WA BANDARI IONGEZWE-CCM

09 July 2023
Share

Halmashauri kuu ya CCM, imekutana leo Julai 09, 2023, katika kikao cha kawaida, kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika katika ukumbi wa White House, uliopo Jijini Dodoma, ambapo kimejadili mambo mbalimbali ikiwemo mkataba wa makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World (DP World) katika uwekezaji na uendeshaji wa bandari.
.
Akitoa taarifa hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bi.Sophia Mjema, amesema katika suala hilo, Halmashauri hiyo imeazimia kuwa Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari.