Back to top

YANGA KUMSHUSHA BEKI HATARI WA UGANDA KESHO

10 July 2023
Share

Klabu ya Soka ya Yanga, kesho Julai 11, 2023, inatarajiwa kumshusha beki wa kati, Gift Fred, akitokea nchini Uganda, huku ikitajwa kuwa klabu hiyo imetumia karibu Tsh. Mil. 115, kuipata saini ya beki huyo machachali na imempa kandarasi ya miaka mitatu. 
.
Beki huyo ambaye amekuwa na kiwango bora akiwa na timu ya SC Villa ya nchini Uganda kwa misimu miwili, pia amepewa nafasi karibu mechi 7 na Kocha Micho Sredojevic wa Timu ya Taifa ya Uganda, amewavutia Yanga, haswa katika michuano ya kufuzu AFCON na kuwafanya wampe mkataba wa miaka mitatu.