Back to top

WAULIZA ZIMAMOTO JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASON NA KUTAFUTA WACHUMBA

10 July 2023
Share

Jeshi la Zimamoto mkoani Mwanza limewaonya baadhi ya Wananchi mkoani humo ambao wamekuwa wakitumia namba ya dharula ya Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uongo na mizaha, ikiwemo kuuliza utaratibu wa kujiunga na mtandao wa Freemason na kutafuta wachumba, hali ambayo Jeshi hilo limedai kuwa imekuwa ikisababisha usumbufu na kuwanyima fursa wanaohitaji msaada wa dharula.
.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Zimamoto, mkoani humo, Mrakibu wa Zimamoto na Uokoaji, Kamila Labani, baada ya kuwavisha vyeo Askari 20 wa Jeshi hilo waliopandishwa vyeo na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.