Back to top

WANANCHI WATOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA POLISI

11 July 2023
Share

Wananchi wa msitu wa Tembo na Londoto, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, wamekabidhi msaada wa pikipiki kwa Jeshi la Polisi mkoani humo, ili kulisaidia  kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya uhalifu ukiwemo wa dawa za kulevya na ukatili wa kijinsia uliokithiri mkoani humo.
.
Akipokea msaada huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi, amewashukuru wananchi hao, ambapo amewataka kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyosaidia kupunguza uhalifu kwenye Mkoa huo.