
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Tanga, Bw. Rajab Abdurahman amewataka viongozi na Makada wa Chama hicho kuacha kuwatolea lugha chafu viongozi wa vya upinzani, badala yake washindane nao kwa kuwaletea maendeleo wananchi kwenye maeneo yao.
.
Mwenyekiti huyo ametoa rai hiyo, wakati akiwahutubia wakazi wa Kata ya Mnyanjani iliyopo Jijini Tanga, baada ya kufungua tawi CCM kwenye Kata hiyo, ambapo pia alipokea kadi ya uanachama ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Bw.Julius Haule, ambaye amejiunga na CCM.
