Back to top

MBARONI KWA KUFUMWA NA BINTI WA MIAKA 12

12 July 2023
Share

David Luya mwenye umri wa miaka 33, mwenyeji wa Mkoa wa Singida amekamatwa na Jeshi la Polisi, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, akituhumiwa kumtumikisha kingono, binti wa miaka 12, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza, katika nyumba aliyopanga, iliyopo eneo la Nazareth, ambapo alipohojiwa na alidai kuwa binti huyo aliingia chumbani kwake kuchukua simu ili awasiliane na Dada yake.
.
Akizungumza na ITV baada ya kumkamata kijana huyo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Wakili Julius Mtatiro, amesema kuwa wamemuhoji binti huyo na amekiri kutumikishwa kingono na kijana huyo, huku vipimo vya hospitali navyo vikithibitisha binti huyo kufanyiwa vitendo hivyo.