
Watu 6 wamefariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari dogo la abiria aina ya Hiace, lenye namba za usajili T 766 DQP lililokuwa likitokea wilayani Bukombe, mkoani Geita, kuelekea Ngara mkoani Kagera, baada ya gari hilo kugongana na uso kwa uso na lori la mizigo lililokwa likitokea nchini Rwanda kuelekea Kenya, katika eneo la Runzewe, huku ikidaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Hiace kusinzia, kisha kuhama upande wake na kulifuata lori.
