Back to top

MAPATO YA TWITTER YAPUNGUA KWA 50% - ELON MUSK

17 July 2023
Share

Mmiliki wa Twitter, Elon Musk amesema mapato ya kampuni hiyo yameshuka kwa 50%, kutokana na kupungua kwa matangazo na madeni makubwa yanayoikumba kampuni hiyo.
.
Bilionea huyo alitoa kauli hiyo wakati akimjibu mmoja wa watumiaji wa mtandao huo, aliyekuwa akimpa ushauri juu ya uendeshaji wa kampuni hiyo.
.
Ikumbukwe kuwa mmiliki huyo wa Twitter, ambaye pia ni mmiliki wa makampuni ya Tesla na SpaceX, alipunguza nusu ya Wafanyakazi wa Twitter, muda mfupi tu baada ya kuinunua kampuni hiyo, kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji.