
Serikali nchini Kenya imeagiza Shule za Msingi na Upili, zilizopo Jijini Nairobi na Mombasa, kufungwa, ambapo imebainisha kuwa imechukua hatua hiyo, baada ya kupata taarifa za kijasusi, juu ya baadhi ya watu waliopanga kushambulia shule katika Kaunti hizo mbili, kupitia maandamano yaliyoitishwa na upinzani nchini humo.
.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Prof.Kithure Kindiki na pamoja na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, ambapo Waziri wa Elimu amebainisha kuwa watatangaza tena kuanza kwa masomo kwenye shule hizo, baada ya kutathminiwa kwa hali ya usalama.
