Back to top

BIL. 22.9 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA RUVUMA

24 July 2023
Share

Mkoa wa Ruvuma umepokea kiasi cha Shilingi Bil. 22.9 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ikiwemo eneo la ununuzi wa dawa na vifaa tiba pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ili kuondoa changamoto ya huduma kwa wananchi. 
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, akiwa katika ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ya kukagua miradi mbalimbali katika Mkoa wa Ruvuma , huku akibainisha kuwa wakati Serikali ya awamu ya 6 inaingia madarakani, ni hospitali mbili tu zilikuwa na huduma za CT-SCAN nchi nzima ikilinganishwa na sasa ambapo hospitali zote za Rufaa za Mikoa zinatoa huduma hiyo.