
Jeshi la Polisi, Mkoa wa Mwanza limesema tayari limemkamata Dereva wa gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin, lenye namba za usajili T 476 DZL, Bw.Oswald Kaijage, lililosababisha vifo vya watu 6 na majeruhi 16, waliokuwa wakifanya mazoezi katika eneo la Lumala lililopo kwenye Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza, siku ya Jumamosi ya Julai 22, 2023.
.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi hilo, mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa, alipofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekoture kuwaona majeruhi wa ajali hiyo, huku akibainisha kuwa Jeshi hilo linaandaa utaratibu utakaosaidia kuwatambua na kuwaelimisha watu wanaofanya mazoezi katika maeneo ya barabara.