Back to top

RUTO YUPO TAYARI KWA MAZUNGUMZO NA ODINGA

26 July 2023
Share

Rais wa Kenya William Ruto, amesema yupo tayari kukutana ana kwa ana kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, wakati wowote.

Rais Ruto ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo hatua hii inakuja baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali, ambayo yamezua taharuki ndani ya nchi hiyo na Kimataifa.