
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), imeutaarifu umma kuwa Sheria ya Fedha, 2023, imefanya marekebisho ya kima cha usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kwa kuongeza kima hicho na kufikia Tsh. Mil. 200/=, kutoka kiwango cha awali cha Tsh. Mil. 100, kilichoanzishwa mwaka 2014.
.
Utekelezaji wa hitaji hilo umeanza Julai 01, 2023, ambapo walipakodi wote ambao wamepata mauzo ya Tsh. Mil. 200/=, kwa mwaka, kwenye mauzo yanayotozwa kodi, wametakiwa kutuma maombi ya usajili wa VAT.
.
Aidha TRA imewataka wafanyabiashara waliokwisha sajiliwa, wenye mauzo chini ya Tsh. Mil. 200/= kwa mwaka, kuomba kusitisha usajili wa VAT na kuwasilisha ritani ya mwisho ya VAT baada ya kufanya marekebisho kwa bidhaa za biashara walizonazo mkononi wakati wa kusitishwa kwa usajili wa VAT.
