Back to top

HIFADHI YA RUAHA YAWAKOSHA WATALII WA NDANI NA NJE

29 July 2023
Share

Watalii wa ndani na nje ya nchi wameendelea kuvutiwa na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kutokana na vivutio vingi kwenye hifadhi hiyo, hususan uwepo wa makundi makubwa ya wanyama jamii ya paka, kama Simba, ambao hukaa zaidi ya 40 kwenye kundi moja, Utalii wa Usiku na Mchana pamoja na Utalii wa Miguu hali ambayo huwafanya watalii hao kukaa kwenye hifadhi hiyo kwa zaidi ya siku moja.


Akizungumzia Hifadhi hiyo, Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Godwell Ole Meng'ataki, amebainisha kuwa Hifadhi hiyo imekuwa kimbilio la watalii wengi kutokana na Utajiri wake wa vivutio.
.
Aidha baadhi ya watalii hao wakiwa hifadhini hapo wamesema imekuwa ni zaidi matarajio kwa kuwa licha ya kuona makundi makubwa ya Simba, pia wameweza kuona wanyama wakubwa na wadogo, ndege zaidi ya aina 570 na mimea ya kila aina. 


Aidha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Godwell Ole Meng'ataki, ameongeza kuwa Hifadhi hiyo ya pili kwa Ukubwa nchini,  imekuwa kivutio kikubwa kutoka kuwa na Miundombinu mzuri hususani baraba ndani ya Hifadhi kupitia Mradi wa kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).
.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Godwell Ole Meng'ata ameongeza kuwa, kupitia Mradi huo wa REGROW, Hifadhi hiyo inatekeleza ujenzi wa Kiwanja Cha ndege, Barabara ndani ya Hifadhi, Uchimbaji wa Mabwawa 32 kwa ajili ya Wanyama, ujenzi wa sehemu za Malazi, Kituo cha Utafiti, Sehemu Kwa ajili ya Ulinzi wa Maliasili nk.