Back to top

WAJAWAZITO MSIKAE MAZINGIRA YANAYOWALETEA MSONGO WA MAWAZO

03 August 2023
Share

Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Dkt.Godwin Mollel, amewataka wajawazito, kukaa katika mazingira yasiyowaletea msongo wa mawazo katika kipindi chote cha ujauzito na unyonyeshaji ili kufanya maziwa yatoke vizuri na mtoto kupata lishe bora na kukua vizuri.
.
Dkt.Mollel ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Unyonyeshaji iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo za Wizara hiyo, zilizopo mkoani Dar es Salaam, ambapo ameendelea kubainisha kuwa mama mjamzito anahitaji matunzo kwaajili ya lishe ya mtoto katika siku 1000 Yaani tangu kutungwa kwa mimba hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili kwani ndio msingi bora wa ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.