
Timu ya soka ya Yanga SC imetangaza kuzindua Documentary itakayoelezea mafanikio ya timu hiyo katika msimu wa mwaka 2022/23, siku ya jumatatu, ya Agosti 7, 2023, katika ukumbi wa sinema wa Century Cinemax, uliopo Dar Free Market, mkoani Dar es Salaam.
.
Akitoa taarifa hiyo Afisa Habari wa timu hiyo Bw.Ally Kamwe, amebainisha kuwa Documentary hiyo itakuwa na kila taarifa na tukio, lililotokea kwenye timu hiyo katika msimu wa mwaka 2022/23.

Kamwe amebainisha kuwa lengo la timu hiyo kuzindua Documentary hiyo, ni kuhakikisha vizazi vijavyo vinakuwa na ushahidi kuwa timu hiyo iliwahi kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
