
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe.Mizengo Pinda, amewataka watanzania kutobeza fursa ya uwekezaji, hususani katika bandari zilizopo nchini, kwani uwekezaji huo utawezesha kupanua wigo, katika maendeleo ya Taifa.
.
Mhe.Pinda ameyasema hayo, alipotembelea maonyesho ya wakulima ya Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya, ambapo ameishauri serikali kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu umuhimu wa uwekezaji huo.
.
Aidha, Meneja Uhusiano na Mawasiliano, Mamalaka ya Bandari nchini (TPA), Bw.Nicodemus Mushi, akabainisha kuwa Mamlaka hiyo inaendelea na mipango ya kuboresha bandari mbalimbali nchini zikiwemo bandari za Ziwa Nyasa.
