Back to top

WASIMAMIZI NEC WAZINGATIE KATIBA YA NCHI.

08 August 2023
Share

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Mhe.Jacobs Mwabegele amewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuzingatia katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na kanuni  zake, Maadili ya Uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na haki.

Jaji Mwambegele ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo kwa Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi leo tarehe 08 Agosti, 2023 mkoani Morogoro ikiwa sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na Kata sita za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 19 Septemba, 2023.

Uchaguzi huo utafanyika katika Jimbo la Mbarali na kata zitakazofanya uchaguzi huo ni: 
Kata ya Nala iliyopo halmashauri ya Jiji la Dodoma, Kata ya Mfaranyaki iliyopo halmashauri ya Manispaa ya Songea, Kata ya Mwaniko iliyopo halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Kata ya Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Rombo, Kata ya Mtyangimbole iliyopo halmashauri ya wilaya ya Madaba na Kata ya Old Moshi Magharibi iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Moshi.