Jeshi la Polisi, Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo nchini, limetoa elimu kwa viongozi wa Wafugaji kutoka mikoa ya Arusha na Manyara, wanaozunguka Hifadhi za Taifa za Wanyama, kuhusiana na namna bora ya kuepuka migogoro ya malisho wakati wa kiangazi, na kuwataka wafugaji kutumia kipindi hiki, ambacho hakina ukame kujiandaa vyema na kutenga maeneo ya malisho, ambayo watayatumia kipindi cha kiangazi.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU), Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua, ametoa elimu hiyo mapema leo huko katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire Mkoani Manyara.
