Back to top

79% YA WALIOJIUA MAREKANI 2022, NI WANAUME.

11 August 2023
Share

Marekani imeweka rekodi ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu waliojiua mwaka jana, ambapo zaidi ya watu 49,000 walijiua mnamo 2022, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na serikali.

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), vilichapisha data mpya siku ya Alhamisi ambapo takwimu zilionyesha kuwa wanaume walikuwa ni asilimia 79, ya jumla ya idadi ya watu waliojiua mnamo 2022.

Wataalamu wanaonya kwamba ongezeko hili linaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya mfadhaiko na upatikanaji mdogo wa huduma za afya ya akili.

Makamu Mkuu wa Rais wa Utafiti katika Wakfu wa Marekani wa Kuzuia Kujiua Jill Harkavy-Friedman ameongeza kuwa kichocheo kikuu ni kuongezeka kwa upatikanaji wa bunduki nchini humo.

Uchambuzi wa hivi majuzi wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, ulitumia data ya awali ya 2022 kukokotoa kwamba kiwango cha jumla cha watu waliojiua kwa kutumia bunduki kilipanda mwaka jana hadi kiwango cha juu zaidi na kwa mara ya kwanza, kiwango cha kujiua kwa bunduki miongoni mwa vijana Weusi kilipita kiwango cha vijana weupe, watafiti waligundua.

Hadi sasa watu wengi bado wanaamini kuwa kuomba msaada ni ishara ya udhaifu.