
Baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS), kutangaza kutuma Jeshi lake la dharura ili kurudisha utawala wa kidemokrasia nchini Niger, Jeshi la nchi hiyo limemwambia mwanadiplomasia mmoja wa ngazi ya juu wa Marekani kuwa, watamuua Rais aliyeondolewa madarakani, Mohammed Bazoum iwapo nchi jirani zitajaribu kuivamia nchi hiyo kijeshi.
.
Taarifa hizo zilizoripotiwa na @dw_kiswahili, zinafuata ikiwa ni muda mfupi tu tangu Viongozi wa ECOWAS wafikie uamuzi huo, ambao pia umeungwa mkono na mataifa ya Marekani na Ufaransa, huku ikitajwa kuwa mataifa hayo mawili yana maslahi makubwa na ya moja kwa moja kwenye Taifa la Niger.
