Back to top

WAPENI MOTISHA WATOA HUDUMA ZA AFYA

11 August 2023
Share

Viongozi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini wametakiwa kutoa motisha kwa wafanyakazi wanaofanya vizuri ili kuwapa ari ya kufanya kazi kwa bidii ya kutoa huduma bora kwa jamii.
.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, kutoka TAMISEMI, Dkt.Ntuli Kapologwe, katika kikao cha majumuisho ya ziara ya tathmini na ukaguzi katika Mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza
.
Dkt.Kapologwe, amefafanua kuwa zawadi sio fedha ,pekee bali wanaweza kuweka utaratibu wa kutoa vyeti au kuwaandikia barua za pongezi na kutambua michango yao kwenye sekta.